Wito wa fursa ya kutuma maombi ya YAI Champion Fellowship.
Kuhusu Young & Alive:
Young and Alive Initiative (YAI) ni shirika lisilo la faida linaloongoza na vijana na wanaharakati wa maendeleo kwa jamii, likiwa na makao yake Dar es Salaam, Tanzania, lililoanzishwa mwaka 2015 na kusajiliwa rasmi mwaka 2017 chini ya namba ya usajili 00NGO0009083. Mbinu ya Young and Alive Initiative ni kuwekeza katika vipaji na stadi za vijana kupitia Ubunifu, Sanaa, na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) ili kusaidia upatikanaji wa huduma na taarifa sahihi za Afya ya Uzazi na Haki za Vijana nchini Tanzania. Shirika linajitahidi kukuza Afya ya Uzazi na usawa wa kijinsia kwa lengo la kufikia maendeleo endelevu nchini Tanzania.
Kuhusu YAI Champion Fellowship Cohort 2 (2023/2024)
YAI CHAMPION FELLOWSHIP ni programu maalum kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15-25. Inawasaidia kujifunza stadi muhimu na kuwa viongozi imara katika eneo la Afya ya Uzazi na Haki za Vijana. Tofauti na awamu ya kwanza, awamu ya pili itafanyika kwa ushirikiano wa Young & Alive Initiative na taasisi ya Tunaweza Organization na Taasisi ya Uongozi ya Bujari na itajikita katika uwajibikaji wa kijamii unaongozwa na vijana kupitia Global Financing Facility (GFF) kuhusu Afya ya Uzazi na Mtoto mchanga (RMNCAH-N) nchini Tanzania.
Jinsi Inavyofanya Kazi
1. Vijana watakao chaguliwa:
Jumla ya vijana (Youth champions) 20 wa YAI kutoka mikoa mitano watachaguliwa kwa njia ya uwazi. Watahiniwa watachaguliwa kulingana na sifa zao. Kamati ya uteuzi itazingatia maarifa, stadi, na shauku ya watahiniwa katika uongozi wa jamii kuhusu masuala ya afya ya uzazi na uzazi.
● Mafunzo
Watakaofuzu na kuchaguliwa watapatiwa mafunzo kuhusu uongozi kwenye sekta ya afya, afya ya uzazi na njia za uwajibikaji wa kijamii unaongozwa na jamii yenyewe.
● Ufuatiliaji/ulezi (Mentroship)
Baada ya mafunzo, washiriki watapata usimamizi na msaada wa karibu wa kuendelea kushirikiana na vijana wenzao kupitia matukio ya ufuatiliaji wa kijamii yenye kuweka alama za matokeo na kupitia jukwaa la mtandaoni www.manju.health , pamoja na kushiriki katika mikutano ya kamati za utawala za vituo vya afya katika maeneo yao.
2. Vigezo vya kuchaguliwa kwenye program:
● Umri wa miaka 18-25 kabla ya kuanza kwa programu. ● Vijana wanawake na vijana wenye ulemavu wanahimizwa kuomba kwa kiasi kikubwa.
● Lazima uwe kijana Mtanzania kutoka mikoa ifuatayo: Mtwara, Njombe, Ruvuma, Mbeya, na Tabora.
Maarifa na uzoefu.
● Uzoefu wa kufanya kazi au kujitolea katika asasi zisizo za kiserikali.
● Uzoefu katika kuratibu shughuli za vijana na hasa zinazohusu kujitolea.
● Uzoefu wa kufanya kazi na makundi tofauti ya kijamii vijana, wanawake, washika dau na watumishi wa serikali.
● Ufahamu wa masuala ya TEHAMA na matumizi yake.
● Uwezo mkubwa wa kujenga mahusiano chanya na vijana rika.
● Maarifa ya kimawasiliano kati yake binafsi na watu wengine.
● Ufahamu au uelewa wa masuala ya afya ya uzazi. Hii ni sifa ya zaida.
● Ufahamu wa (RMNCAH-N). Hii ni sifa ya ziada.
Majukumu ya kufanya.
Mipango na usimamizi wa kazi:
● kupanga na kusimamia shughuli za mradi katika ngazi ya wilaya, ikiwa ni pamoja na vikao, warsha, mazungumzo, na shughuli za kujieleza kwa ubunifu.
● kushiriki katika bodi za utawala wa vituo vya afya ngazi ya halmashauri moaka ngazi ya jamii.
● kuhakikisha mambo ya logistiki kwa matukio ya kikanda yanakwenda vizuri.
Logistiki na Uhamasishaji wa Vijana:
● kuhamasisi na kushirikisha vijana ndani ya wilaya kushiriki kikamilifu katika mazungumzo ya jamii.
● kutoa suluhisho zinazotokana na vijana, ubunifu, na mazoea bora kupitia
Majukwaa la Manju Tanzania (www.manju.health).
● Kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchechemuzi kwa vijana kuhusu uwajibikaji wa kijamii katika vituo vya afya.
Mawasiliano na Uandishi wa ripoti:
● Kutoa sasisho na ripoti za kuhusu shughuli katika ngazi ya wilaya kwa timu ya uongozi wa mradi.
● Kutoa na kuripoti mwenendo bora, changamoto, na taarifa za mafanikio kutoka katika shughuli za jamii zinazofanyika.
● Kushirikiana na vijana wenzako wa halmashauri zingine ili kutoa mafanikio na ufahamu wa matukio na shughuli za mradi.
● Kuhusika kwa wakati katika kuwasiliana na kutoa taarifa yoyote kuhusu mahitaji na mipango ya mradi kwa Mratibu wa Mradi.
● Ripoti kwa wakati kuhusu shughuli zilizofanyika ili kuelewa nini kilifanya kazi, nini hakukufanya kazi, na nini kinaweza kuboreshwa katika jitihada za baadae.
Muda wa utekelezaji mradi:
Youth Champions watakuwa na jukumu la kuwa kwenye mradi huu kwa miezi nane (8), kuanzia November 2023 hadi Julai 2024.
Malipo:
Hii ni nafasi ya kujitolea. Hata hivyo, Youth Champions watapokea posho za kila mwezi ili kusaidia shughuli zao kwenye maeneo watakayofanyia kazi, ikiwa ni pamoja na kusaidia kwa usafiri na malazi wakati wa kutimiza majukumu yao.
Jinsi ya kutuma maombi:
Vijana walio na nia wanapaswa kujaza na kuwasilisha Fomu ya Maombi ya mtandaoni KWA HAPA, pamoja na wasifu wako binafsi (CV)
ifikapo Jumatano, Oktoba 18. (DEADLINE IMESOGEZWA MBELE HADI 20 OKTOBA, SAA 5:59.
Young & Alive Initiative natoa nafasi kwa kujumuisha makundi yote ya vijana Tanzania. Tunahimiza maombi kutoka kwa watu wa asili zote, hasa wale wanaotoka katika jamii ambako mradi unafanyika na kwa watu wanaoishi na ulemavu.
Zingatia: Vijana waliochaguliwa pekee watapewa taarifa na kuitwa kwa ajili ya usaili.
Wasiliana Nasi:
Ikiwa una maswali au wasiwasi wowote, tafadhali wasiliana nasi kupitia namba 0621053133 au kwa barua pepe kwa elibarick@youngandalive.org kwa masaa ya kazi pekee.
.
Comments